WANANCHI WATAKIWA KUZINGATIA TAARIFA YA HALI YA HEWA

WANANCHI WATAKIWA KUZINGATIA TAARIFA YA HALI YA HEWA

Like
188
0
Tuesday, 01 September 2015
Local News

WATANZANIA wametakiwa kufuatilia na kuzingatia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa nchini-TMA– ili kuepukana na athari zitokanazo na mabadiliko ya hali hewa.

 

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo dokta Agnes Kijazi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika warsha ya siku moja juu ya Elnino na kusema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa huweza kuleta athari mbaya kwa jamii.

 

Dokta Kijazi amesema kuwa Elnino husababishwa na ongezeko la joto katika bahari ya Pasifiki jambo ambalo husababisha ongezeko la joto katika bahari za Atlantiki na Hindi na kusababisha mvua nyingi zenye madhara.

Comments are closed.