WANANCHI WATOA MAONI TOFAUTI KUFUATIA MAAMUZI YA LOWASSA

WANANCHI WATOA MAONI TOFAUTI KUFUATIA MAAMUZI YA LOWASSA

Like
189
0
Wednesday, 29 July 2015
Local News

BAADA  ya jana kutangaza rasmi kuachana na chama cha Mapinduzi –CCM kwa aliyekuwa kada na mwanachama wa muda mrefu wa chama hicho, Edward Lowasa, na kuunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA, baadhi ya Wananchi Jijini Dar es salaam wamekuwa na maoni mbalimbali kufuatia uamuzi huo.

 

Wakizungumza na kituo hiki kwa nyakati tofauti Wananchi hao wamesema uamuzi aliochukua Lowasa ni mzuri na wanauunga mkono kwa kuwa maamuzi hayo yatasaidia kukuza siasa ya vyama vingi na hivyo kukuza demokrasia.

 

Aidha Baadhi ya Wananchi wamekuwa na maoni tofauti na uamuzi huo ambapo wamebainisha kuwa sio uamuzi wa busara kwa kuwa unaonesha kuwa nia yake inatawaliwa na uchu wa madaraka.

 

Comments are closed.