WANANCHI WENYE UWEZO WAHIMIZWA KUWEKEZA KWENYE VINU VYA MAZAO YA KILIMO

WANANCHI WENYE UWEZO WAHIMIZWA KUWEKEZA KWENYE VINU VYA MAZAO YA KILIMO

Like
456
0
Tuesday, 11 November 2014
Local News

WANANCHI wenye uwezo wamehimizwa kuwekeza kwenye vinu vya mazao ya kilimo ili kuweza kuwasaidia wakulima kuwapa uhakika wa masoko yao.

 

Ushauri huo umetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji DOKTA MERRY NAGU katika ziara yake ya kutembelea viwanda mbalimbali nchini, na kusema uwekezaji huo utawasaidia wakulima walime zaidi kwakuwa viwanda vinauwezo wakutunza vyakula kwa utaalam na usalama wa kutosha.

 

DOKTA NAGU amesema uzalishaji wa nafaka umeongezeka kutokana na serikali kutoa zana za kilimo ikiwemo pembejeo na matrekta hivyo viwanda hivyo ni muhimu kwani mbali na kuwa na uhakika wa utunzaji wa nafaka pia wanatengeneza ajira nchini.

Vitalu vya TAHA na Barton Tanzania

 

Comments are closed.