WANAOPANDISHA NAULI KIHOLELA TEGETA WAPIGWA MARUFUKU KUTOA HUDUMA YA USAFIRI

WANAOPANDISHA NAULI KIHOLELA TEGETA WAPIGWA MARUFUKU KUTOA HUDUMA YA USAFIRI

Like
321
0
Monday, 13 April 2015
Local News

KUFUATIA Malalamiko ya Wananchi wa Mbezi Mwisho kata ya Tegeta A kuhusu kupandishwa kwa nauli za daladala kiholela hasa nyakati za asubuhi na jioni Serikali ya Mtaa huo imepiga marufuku magari yote yanayopandisha nauli kuendelea kutoa huduma ya usafiri.

Akizungumza katika Mkutano na Wananchi wa Kata hiyo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tegeta A Marko Maginga amesema imekuwa ni desturi ya magari yanayotoa huduma ya usafiri kutoka Mbezi mwisho kwenda Goba mpakani katika eneo hilo la Tegeta A kupandisha nauli kuwa shilingi elfu moja badala ya shilingi miatano ya kawaida jambo ambalo limekuwa likileta usumbufu mkubwa kwa wananchi hao na kufikisha malalamiko hayo ofisi ya serikali ya mtaa.

Maginga amesema baada ya ofisi yake kupokea malalamiko hayo imewaita madereva na kuwataka kutoza nauli ya kawaida ya shilingi miatano na asietaka kutoza nauli hiyo basi asiendelee kutoa huduma hiyo ya usafiri kwani kupandisha nauli ni kusababisha usumbufu kwa wananchi.

Comments are closed.