WANAOWANIA TIKETI REPUBLICAN WAJIBIZANA VIKALI

WANAOWANIA TIKETI REPUBLICAN WAJIBIZANA VIKALI

Like
177
0
Thursday, 29 October 2015
Global News

WANAOWANIA nafasi ya kuwania urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican jana wamejibizana vikali kwenye mdahalo wa tatu ulioandaliwa katika jimbo la Colorado.

Donald Trump na Ben Carson, ambao hawana uzoefu mkubwa kisiasa lakini ndio wanaoongoza kinyang’anyiro hicho, wameshambuliwa kwenye mdahalo huku Gavana wa Ohio John Kasich akiukashifu mpango wake “wa ndoto kuhusu ushuru”.

Hata hivyo Pendekezo lake kuhusu ushuru, lilishutumiwa vikali na Kasich, ambaye pia alishutumu vikali mpango wa Trump wa kuwaondoa wahamiaji milioni 11 kutoka Mexico na kujenga ukuta kwenye mpaka wa taifa hilo na Mexico.

Comments are closed.