WANASIASA WATAKIWA KUWA NA MSIMAMO NA VYAMA VYAO

WANASIASA WATAKIWA KUWA NA MSIMAMO NA VYAMA VYAO

Like
194
0
Tuesday, 11 August 2015
Local News

KUFUATIA matukio kadhaa ya wanasiasa kuvihama vyama vyao baada ya kuenguliwa katika kinyang’anyilo cha  kugombea nyadhifa mbalimbali Msanii wa sanaa ya Uigizaji Nchini Steven Mengere amewataka Wanasiasa kuwa na Msimamo ndani ya vyama vyao.

 

Mengere ameyasema hayo wakati akizungumza na kituo hiki  na kudai  kuwa mfumo huo umekuwa ndio kimbilio la Wanasiasa wanaokosa sifa za kugombea kupitia vyama vyao wakidhani kwamba hiyo ndio njia ya kupata uongozi.

 

Amebainisha kuwa  pamoja na kushindwa katika kinyang’anyilo hicho ni vyema kwa viongozi hao kuwaunga mkono washindi ili kuendeleza jitihada za kuleta maendeleo kwa Taifa.

 

Comments are closed.