WAZAZI hususani wakina baba wameaswa kushiriki katika Malezi ya Watoto ili wawajenge watoto na wakue katika fikra bora zitakazowapa amani, furaha na matumaini ya maisha yao.
Hayo yamesemwa leo na Afisa Uhusiano wa Shirika linaloshughulikia Masuala ya watoto la SAVE THE CHILDREN INTERNATIONAL ELLEN OTARU OKOEDION wakati akizungumza na EFM juu ya namna Wazazi wanavyoweza kumlea mtoto katika malezi bora.