WANAWAKE MARA WAASWA KUSHIRIKIANA

WANAWAKE MARA WAASWA KUSHIRIKIANA

Like
265
0
Monday, 05 October 2015
Local News

WANAWAKE Mkoani Mara wameaswa kushirikiana kwa pamoja katika shughuli za maendeleo bila kujali tofauti zao za vyama ili kujiletea maendeleo.

 

Rai hiyo imetolewa na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wanawake wa mkoa huo juu ya umuhimu wa ushirikiano katika shughuli mbalimbali.

 

Mama Salma ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi mjini amesema kuwa masuala yanayowahusu  wanawake hayana itikadi za vyama kwani maendeleo ni ya wote.

Comments are closed.