WANAWAKE TANGA WATAKIWA KUJITOKEZA NA KUCHANGAMKIA FURSA

WANAWAKE TANGA WATAKIWA KUJITOKEZA NA KUCHANGAMKIA FURSA

Like
350
0
Wednesday, 29 October 2014
Local News

WANAWAKE wajasiriamali mkoani Tanga wametakiwa kujitokeza na kuchangamkia fursa zitakazotolewa na kampeni ya mwanamke na uchumi inayotarajiwa kutolewa mwanzoni mwa mwezi ujao mkoani Tanga ambapo zaidi ya wanawake 300 watanufaika na mafunzo hayo yanayotolewa na kampuni ya Angels Moment ya jijini Dar Es Salaam.

Mkuu wa wilaya ya Tanga Mheshimiwa Halima Dendego amesema fursa zitakazotolewa ni fahari kwa wanawake na wajasiriamali wa mkoa huo kwani elimu inahitajika sana wakati huu wa ushindani wa biashara.

 

Mkuu huyo wa wilaya amewaomba Wadau mbalimbali waendelee kujitokeza kuunga mkono juhudi za Kampeni ya mwanamke na uchumi kwani kupitia akina mama huduma zao zitaweza kufahamika na kunufaika kwani ndiyo nafasi pekee ya kukutana na wajasiriamali na kusaidia kuinua uchumi wa akinamama na Taifa kwa ujumla.

 

 

 

 

Comments are closed.