WANAWAKE WAJAWAZITO WAMESHAURIWA KUFUATA KANUNI ZA AFYA

WANAWAKE WAJAWAZITO WAMESHAURIWA KUFUATA KANUNI ZA AFYA

Like
319
0
Wednesday, 18 November 2015
Local News

WANAWAKE wajawazito nchini wameshauriwa kufuata kanuni bora za Afya ikiwemo kuhudhuria Hospitalini mara kwa mara ili waweze kuepuka kujifungua watoto njiti.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha  maadhimisho ya siku ya watoto waliozaliwa kabla ya miezi 9, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick amesema kuwa endapo wanawake watatimiza lengo la kuhudhuria Hospitalini na kufuata ushauri wanaoupata kutoka kwa madaktari kuna uwekano wa tatizo hilo kupungua.

Aidha, Sadick amewataka wanaume kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wake zao wakati wote wake zao wanapokuwa na uja uzito ili kusaidia kupunguza tatizo hilo.

Comments are closed.