WANAWAKE WALIOCHAGULIWA KATIKA NAFASI ZA UONGOZI WAMETAKIWA KUWAJIBIKA KIKAMILIFU

WANAWAKE WALIOCHAGULIWA KATIKA NAFASI ZA UONGOZI WAMETAKIWA KUWAJIBIKA KIKAMILIFU

Like
250
0
Wednesday, 11 November 2015
Local News

MTANDAO wa Jinsia Tanzania-TGNP-pamoja na wanaharakati wa ngazi ya jamii wamewataka wanawake waliochaguliwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi kuwajibika kikamilifu kwa kuitumikia jamii kwani ndiyo iliyowapa ridhaa.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam jana na mkurugenzi wa-TGNP- Bi. Lilian Liundi wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mchakato wa uchaguzi kuanzia hatua ya awali hadi mwisho lengo ikiwa ni kuangalia ushiriki wa wanawake kwenye uchaguzi.

LIUNDI amebainisha kuwa kulingana na ahadi walizozitoa viongazi wateule wakati wakiomba kura wana imani kuwa viongozi hao watasimamia vyema ahadi hizo kwa manufaa ya Taifa.

Comments are closed.