WANAWAKE WATAKIWA KUJITOKEZA KUWANIA NAFASI MBALIMBALI KATIKA VYAMA VYA SIASA

WANAWAKE WATAKIWA KUJITOKEZA KUWANIA NAFASI MBALIMBALI KATIKA VYAMA VYA SIASA

Like
186
0
Tuesday, 14 July 2015
Local News

CHAMA cha Sauti ya Umma kimewataka wanawake wenye uwezo wa uongozi kujitokeza katika kuwania nafasi mbalimbali kwenye vyama vya siasa  na  kuleta uwiano sawa wa  hamsini kwa hamsini katika uongozi hapa nchini ili kuiondoa asilimia 30 iliyopo sasa.

 

Akizungumza na kituo hiki Katibu Mkuu wa Chama hicho Ally Kaniki amesema kuwa wapo wanawake wenye uwezo mkubwa wa kuongoza lakini wamekuwa nyuma na kushindwa kuthubutu kutokana na uoga na kutokujiamini.

 

Aidha amewataka wanawake kote nchini kuondoa dhana ya kusubiri kuteuliwa viti maalum kwani hatua hiyo haiwezi kuwajengea ukomavu wa kisiasa na utendaji bora wa kazi zao.

Comments are closed.