WANAWAKE nchini wamehimizwa kuachana na malumbano na badala yake wameshauriwa kuondoa hofu na kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa ndani na nje ya chama katika ngazi za mikoa na Taifa lakini pia wajitokeze kuomba nafasi ambazo zitawaniwa kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu .
Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mabadiliko na Uwazi-ACT, MOHAMED MASSAGA kwenye sherehe ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyoadhimishwa jana Machi 8.
Ameesema kuwa Katiba pendekezwa imeondoa kipengele muhimu cha asilimia hamsini kwa hamsini kwa wanawake hali inayochangia wanawake wengi nchini kupoteza nafasi halali ya ushiriki bungeni.