WAZIRI Mkuu wa Uingereza David Cameron anatarajiwa kulaani matumizi ya fedha chafu kutoka maeneo mbalimbali ya dunia zinazotumiwa kununua mali nchini Uingereza.
Katika hotuba anayotarajia kuitoa nchini Singapore muda mfupi ujao waziri Cameron anatarajiwa kuahidi kufichua taarifa ya kutumiwa kwa kampuni za kununua mali za kifahari na kusema kuwa Uingereza haipaswi kuwa mahali pa fedha za wizi.
Zaidi ya mali laki moja za Uingereza zimesajiliwa kwa majina ya kampuni za kigeni na zaidi ya robo ya kampuni hizo zipo jijini London.