WAPALESTINA WANNE WAUAWA UKINGO WA MAGHARIBI

WAPALESTINA WANNE WAUAWA UKINGO WA MAGHARIBI

Like
217
0
Friday, 08 January 2016
Global News

JESHI la Israel limesema kwa Wapalestina wanne wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kujaribu kuwachoma visu wanajeshi wa Israel katika matukio mawili tofauti eneo la Ukingo wa Magharibi.

 

Watatu waliuawa katika makutano ya barabara ya Gush Etzion, ambako visa kama hivyo vimewahi kutokea awali na mwingine aliuawa karibu na Hebron lakini hakuna mwanajeshi aliyejeruhiwa.

 

Maafisa wa afya wa Palestina wamethibitisha vifo hivyo.

Comments are closed.