WAPIGA RAMLI 225 MBARONI KUFUATIA MAUAJI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI

WAPIGA RAMLI 225 MBARONI KUFUATIA MAUAJI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI

Like
244
0
Thursday, 12 March 2015
Local News

JUHUDI za kukomesha matukio ya kihalifu ya kuwaua watu wenye Ulemavu wa

Ngozi Albino, zimeanza kuzaa matunda baada ya Jeshi la Polisi kuwashikilia wapiga ramli 225.

Kushikiliwa kwa wapiga ramili hao kunatokana na Operation inayoendeshwa na Polisi ya kupambana na vitendo vya Kikatili ili kuhakikisha matukio hayo hayaendelei kutokea.

Taarifa iliyotolewa jijini Dar es salaam na Msemaji wa Jeshi la Polisi ADVERA BULIMBA imeeleza kuwa wapiga ramli hao wamekamatwa kwenye Mikoa ya Tabora,Geita,Mwanza,Simiyu,Shinyanga,Kagera,Katavi na Rukwa.

Comments are closed.