WAPIGANAJI WA KIKURDI WASHAMBULIWA

WAPIGANAJI WA KIKURDI WASHAMBULIWA

Like
172
0
Tuesday, 11 August 2015
Global News

NCHI ya Uturuki imeanzisha tena msururu wa mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi yanayolenga maeneo 17 kusini mashariki mkoani Hakkari katika mpaka na Iran.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Uturuki imeshuhudia ghasia zaidi katika wiki za hivi karibuni kati ya wanajeshi na wapiganaji wa Kikurdi wanaotaka kujiondoa katika utawala wa jeshi.

Mashambulio hayo yanajiri siku moja baada ya watu tisa kuuawa katika msururu wa mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama huku wengine wakiwa katika eneo la kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Comments are closed.