WAPIGANAJI WANAOMUUNGA MKONO RAIS WA YEMEN WAUTWAA MJI WA ADEN LEO

WAPIGANAJI WANAOMUUNGA MKONO RAIS WA YEMEN WAUTWAA MJI WA ADEN LEO

Like
277
0
Wednesday, 15 July 2015
Local News

TAARIFA za kijeshi zimesema wapiganaji tiifu kwa upande wa rais wa Yemen wamefanikiwa kuyadhibiti maeneo kadhaa ya mji wa Aden leo, baada ya kuukomboa uwanja wa ndege wa mji huo ambao ulikuwa ukishikiliwa na waasi wa kihuthi kwa zaidi ya miezi minne.

Operesheni hiyo iliyopewa jina “Operesheni ya Mshale wa Dhahabu” ni ya kwanza kupata mafanikio makubwa, tangu wanamgambo wa kihuthi walipoingia mji huo wa bandari na kumlazimisha rais Abedrabbo Mansour Hadi kukimbilia nchi jirani ya Saudi Arabia.

Rais wa Marekani Barack Obama na mfalme Salman wa Saudi Arabia wametaka  mapigano yasitishwe haraka nchini humo.

 

Comments are closed.