WAPINZANI wawili wakuu wa Donald Trump katika kinyang’anyiro cha kumteua mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani wametangaza mipango ya kuungana kukabiliana na mgombea huyo.
Ted Cruz na John Kasich wanataka kushirikiana kupunguza uwezekano wa mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York kushinda mchujo katika majimbo zaidi.
Cruz, ambaye ni seneta wa jimbo la Texas, amesema atapunguza kampeni zake katika majimbo ya Oregon na New Mexico, Kwa upande wake John Kasich, ambaye ni gavana wa Ohio, naye amesema atamwachia Cruz katika mchujo ujao jimbo la Indiana.