WANAUME wawili wamekamatwa kuhusiana na jaribio la shambulizi la kigaidi karibu na eneo la Orleans kusini mwa mji mkuu wa Ufaransa, Paris.
Polisi imesema washukiwa hao walipanga kufanya mashambulizi yanayolenga asasi za kiusalama.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve amesema mashambulizi hayo yaliyotibuliwa na shirika la ujasusi la Ufaransa, yalikusudia kuwalenga maafisa wa usalama katika eneo la Orleans.