WASICHANA 500 WA TANZANIA WANATUMIKA ASIA

WASICHANA 500 WA TANZANIA WANATUMIKA ASIA

Like
320
0
Friday, 10 June 2016
Local News

Serikali imesema zaidi ya wasichana 500 wanatumikishwa katika kazi hatari zikiwemo za ukahaba katika nchi za Asia na Uarabuni.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje imesema imepata taarifa kuwa kuna mtandao unaowasafirisha wasichana katika nchi hizo kwa madai ya kufanya kazi za ndani lakini baadae hutumikishwa kwenye biashara ya ngono.

Taarifa zinasema baadhi ya wasichana hao wemekimbilia kwenye ubalozi wa Tanzania ili kuomba kurudishwa nyumbani

Mindi Kasiga ni Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ambaye anasema ”

Mtandao huo unachofanya ni pamoja na kuwatafuta wasichana wenye umri kati ya miaka 18 na 24 na hata chini ya umri huo na kuwalaghai kuwa kuna fursa za ajira katika mahoteli, migahawa, maduka makubwa au kazi za nyumbani nchi za nje na kwamba watawasaidia wasichana hao kupata kazi hizo pamoja na kuwawezesha kupata vyeti vya kusafiria VISA na tiketi za ndege kwa ajili ya kusafiri kwenda kwenye nchi husika”.

Wengi wa watu wanaokumbana na ahadi hizo, wanavutika kirahisi kwani wanaona hiyo ni fursa ya kujipatia ajira na kipato cha uhakika.

Kwa taarifa tulizozipata kuhusiana na mtandao huo ni kwamba wengi wa Watanzania wanoenda India,

Hulazimishwa kufanya ukahaba na kunyang’anywa hati za kusafiria ili kuwadhibiti wasitoroke, ndiyo matatizo makubwa zaidi ambayo yamekuwa yakiwakabili Watanzania.

Kufuatia matumaini wanayojengewa na walaghai vijana wa Kitanzania wamejikuta au wamelazimika kukubali kufanya kazi za ukahaba ili kurejesha gharama za kuwasafirisha kutoka Tanzania kwenda katika mataifa hayo ili waweze kurejeshewa Hati zao za kusafiria pamoja na kupata nauli kwa ajili ya kurudi Tanzania.

 

Comments are closed.