WASIRA AAGIZA SUKARI IINGIZWE SOKONI

WASIRA AAGIZA SUKARI IINGIZWE SOKONI

Like
420
0
Thursday, 12 February 2015
Local News

WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mheshimiwa Stephen Wasira, amewaagiza wazalishaji na wafanyabiashara wa sukari nchini, kuingiza Sukari nchini badala ya kuiweka kwenye maghala ili kushusha bei ya bidhaa hiyo muhimu. Agizo hilo la Serikali limekuja ikiwa ni siku chache baada ya kupanda ghafla kwa bei ya sukari kutoka shilingi 1,700 bei ya awali hadi shilingi elfu 3 kwa kilo. Waziri Wasira ametoa kauli hiyo ya Serikali alipokutana na wadau wa Sukari na kutoa tamko la Serikali kuhusu kupanda kwa bei ya sukari nchini.wasira2 wasira3

Comments are closed.