WASOMI NA WAFANYABIASHARA NCHINI WAUNGA MKONO UTEUZI WA MAGUFULI

WASOMI NA WAFANYABIASHARA NCHINI WAUNGA MKONO UTEUZI WA MAGUFULI

Like
290
0
Friday, 11 December 2015
Local News

IKIWA imepita siku moja tokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli atangaze   Baraza jipya la Mawaziri lenye Wizara 19, Mawaziri 18 huku Wizara nne zikiwa bado hazina Mawaziri baadhi ya Wananchi wakiwemo wasomi na Wafanyabiashara wamekuwa na maoni mbalimbali huku wengi wakilipongeza.

 

Akizungumza na Efm jijini Dar es salaam Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dokta Benson Bana amesema kuwa uteuzi uliofanywa ni uteuzi ambao haujangalia uso na majina ya Viongozi bali umeangali zaidi muundo wa Serikali ya awamu ya tano na ndio maana Wizara nyingi zimeunganishwa kuwa Wizara moja ili kuondoa  marudio na kuingiliana kwa majukumu jambo ambalo ni jema kwa kuwa litasaidia kupunguza gharama za Serikali

Comments are closed.