WATAALAM, wa maswala ya uchumi nchini wametakiwa kupima na kutazama kipato cha wananchi wanapofanya tathmini za ukuwaji wa uchumi badala ya kutaja viwango vya ukuaji wa serikali wakati wananchi ni masikini.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa fedha na Mbunge wa Mkuranga Mheshimiwa ADAM MALIMA alipokuwa akifungua warsha ya siku nne, kujadili ripoti ya ukuwaji wa uchumi kwa nchi za Afrika unaofanyika kwa ufadhili wa Benki ya maendeleo ya Afrika ambapo amesema walengwa hasa wa tathimini hizo ni wananchi.