WATAALAMU kutoka Sekta za Nishati na Madini nchini wametakiwa kuwa wabunifu katika maandalizi na Usimamizi wa Miradi ili sekta hizo ziwe na mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Wito huo umetolewa na Kamishna Msaidizi wa Umeme Mhandisi INNOCENT LUOGA kwa niaba ya Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Mhandisi HOSEA MBISE alipokuwa akifungua mafunzo ya uandaaji wa mapendekezo ya Miradi, Sera na Mbinu za usimamizi wa Miradi.
Mafunzo hayo yamewashirikisha Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini,-TANESCO, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji -EWURA na Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi –TDGC yanayoendelea mjini Bagamoyo.
Mafunzo hayo yanatolewa na Mtaalamu Mwelekezi ambaye ni Kampuni ya Petrogas yenye makazi yake jijini Dar es Salaam.