WATANZA WASHAURIWA KUACHA KUTUMIA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU

WATANZA WASHAURIWA KUACHA KUTUMIA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU

Like
319
0
Wednesday, 27 May 2015
Local News

WATANZANIA wameshauriwa kuwa waangalifu na kuacha tabia ya kuiga matumizi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na mamlaka husika kwa kuwa ni hatari kwa Afya zao.

 

Rai hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu waziri wa wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo mheshimiwa JUMA NKAMIA kwa niaba ya Waziri wa Afya, wakati akijibu swali la mheshimiwa RIZIKI JUMA aliyetaka kufahamu jitihada za serikali katika kudhibiti tatizo hilo nchini.

 

Mheshimiwa NKAMIA amesema kuwa ni vyema kwa kila mwananchi kuchukua jitihada za kutosha kuhakikisha unapatikana uelewa wa kutosha wa kuachana na matumizi ya vipodozi hivyo.

 

Aidha ameeleza kuwa serikali kupitia mamlaka ya chakula na dawa nchini-TFDA- inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kusaidia kudhibiti uzalishaji na usambaaji wa vipodozi vilivyopigwa marufuku ili visifike kwa wananchi.

 

Hata hivyo mheshimiwa NKAMIA ameziomba taasisi zote za kidini kushirikiana vyema na serikali katika kutoa elimu kwa wananchi ili kupunguza kasi ya usambaaji na athari zitokanazo na matumizi ya vipodozi hivyo.

Comments are closed.