Akizungumza katika kongamano la 30 la Kimataifa la Wanasayansi Watafiti jijini Dar es Salaam jana, Mtafiti katika Mradi wa Amani Medical uliopo chini ya Nimr, Said Magogo alisema kufuatia tatizo hilo kituo hicho kipo kwenye mchakato wa kuhakikisha kinapata dawa mbadala.
Alisema mbu hao wanajenga usugu hata kwenye dawa ya kuua mazalia yao inayotumiwa katika vyandarua, hivyo kuishi muda mrefu zaidi. “Mfano Korogwe ambako zimewekezwa nguvu nyingi hasa katika kugawa vyandarua kwa asilimia 80, tunaendelea kuangalia dawa mbadala ambayo tutaitumia kuangamiza mbu hao,” alisema.
Alisema chanzo cha usugu ni aina hiyo ya dawa kutumika muda mrefu, hivyo hata inapotokea mbu akataga mayai tayari yanakuwa na dawa hiyo si rahisi kuuawa.