WATANZANIA KUPAMBANA DENGUE KWA KUTUNZA MAZINGIRA

WATANZANIA KUPAMBANA DENGUE KWA KUTUNZA MAZINGIRA

Like
260
0
Wednesday, 11 March 2015
Local News

WATANZANIA wametakiwa kupambana na ugonjwa wa Dengue kwa kuhakikisha mazingira yanayowazunguka yanakuwa safi ili kupunguza mazalia ya Mbu wanaosababisha ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, Dokta MWELE MALECELA wakati akitoa taarifa ya Utafiti wa Mlipuko  wa Dengue jijini Dar es es salaa uliofanywa na Taasisi yake.

Dokta MALECELA amesema lengo la Utafiti huo ni kukusanya takwimu za kiwango cha maambukizi ya Dengue kwa wagonjwa wanaofika katika vituo vya kutolea huduma za Afya pamoja na kutambua aina za Kirusi anayeambukiza ugonjwa husika.

Comments are closed.