LEO USIKU Watanzania wataungana na wenzao katika baadhi ya maeneo Ulimwenguni kuukaribisha mwaka mpya 2015.
Ni dhahiri kwamba litakuwa ni jambo la kumshukuru Mungu kwani kuuona mwaka mpya si jambo dogo bali ni kwa kudra za Mwezi Mungu.
Katika kuukaribisha mwaka mpya ambapo kawaida shughuli katika maeneo mbalimbali huanza muda wa Saa 6 usiku watu hukusanyika na kufanya sherehe.
Wapo wanaokwenda kwenye nyumba za Ibada,wanaokwenda katika Viwanja mbalimbali ukiwamo uwanja wa Taifa kufanya Ibada ya kumshukuru Mungu kwa kumaliza mwaka salama.