WATANZANIA WAASWA KUSHIRIKI SHUGHURI ZINAZOENDESHWA NA EFM KUTIMIZA NDOTO ZAO

WATANZANIA WAASWA KUSHIRIKI SHUGHURI ZINAZOENDESHWA NA EFM KUTIMIZA NDOTO ZAO

Like
310
0
Thursday, 02 April 2015
Local News

WATANZANIA wameaswa kuendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Kituo cha Radio cha E FM kwa lengo la kuwasaidia kutimiza ndoto zao za maisha ya baadae pamoja na kuliletea Taifa maendeleo.

Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa E FM, FRANCIS SIZA wakati wa hafla ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanza kwa shughuli za urushaji wa matangazo ya Efm Radio.

Hafla hiyo imehudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Meya wa Manispaa ya Kinondoni YUSUPH MWENDA, Mbunge wa Kigoma Kusini Mheshimiwa DAVID KAFULILA, Mheshimiwa ZITTO KABWE Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, na Mkurugenzi wa Masoko kutoka Zantel, SUKHWINDER BAJWA.

Comments are closed.