WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia nafasi mbalimbali zilizopo katika Sekta nzima ya TEHAMA kwa kujitokeza na kuthubutu kujifunza kushiriki kwa ufanisi katika kushindana au kusaidiana na kampuni zinazokuja kutoka nje kwa kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kuboresha na kuendeleza Sekta hiyo kwa kuwa bado ingali changa.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam katika kilele cha mkutano wa CAPACITY Africa ulioshirikisha nchi zaidi ya 65 na kampuni mbali kutoka Ulaya America na Asia kujadili na kujengeana uwezo kuhusu masuala mbalimbali ya TEHAMA yanayoweza kusaidia kuendeleza sekta hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara Sayansi Teknlojia na Mawasiliano John Mngodo amesema jambo la msingi ni Wafanyabiashara wa ndani kuwa na Ujuzi na Taaluma inayohitajika katika sekta hiyo na sio kuwa na ukiritimba.