WATANZANIA WAMETAKIWA KUDUMISHA AMANI KATIKA KIPINDI CHA UCHAGUZI

WATANZANIA WAMETAKIWA KUDUMISHA AMANI KATIKA KIPINDI CHA UCHAGUZI

Like
285
0
Monday, 19 October 2015
Local News

WATANZANIA wametakiwa kuilinda na kuidumisha Amani iliyopo hasa kuelekea kipindi cha Uchaguzi bila kujali itikadi zao za vyama kwani Amani ndiyo msingi wa maendeleo kwa Taifa.

 

Akizungumza na Efm jijini Dar es salaam,  mgombea wa nafasi ya Udiwani kata ya Kunduchi kupitia chama cha mapinduzi-CCM-Michael Urio amesema kuwa ili kila mwananchi awe na uhuru wa kufanya kazi ni muhimu Amani kuwepo.

 

Kwa upande wa wafanyabiashara Urio amebainisha kwamba mara baada ya kupewa ridhaa ya kuongoza kata hiyo atahakikisha anawatengea maeneo maalum wafanyabishara wa kata hiyo ili wanufaike na biashara zao.

Comments are closed.