WATANZANIA WAMETAKIWA KUEPUKA KUANDIKA AU KUTAJA TAKWIMU ZISIZO RASMI

WATANZANIA WAMETAKIWA KUEPUKA KUANDIKA AU KUTAJA TAKWIMU ZISIZO RASMI

Like
247
0
Wednesday, 20 May 2015
Local News

WATANZANIA wametakiwa kuepuka  kuandika au kutaja takwimu zisizo rasmi kwani vitendo hivyo ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria mpya ya takwimu ya mwaka 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu ofisi ya Takwimu Dokta Albina Chuwa amesema takwimu bora husaidia serikali yoyote duniani kupanga mipango ya maendeleo ya wananchi wake hivyo ni bora kuwekwa kwa chombo maalum kinachotoa takwimu kama ilivyo kwa ofisi ya Taifa ya Takwimu.

Ameeleza kuwa ni vyema takwimu rasmi isipotoshwe na chombo chochote cha habari na kifungu hiki kinalenga kuwa takwimu rasmi inayotangazwa ieleze chanzo chake.

Aidha katika Sheria hiyo imebainisha kuwa ni kosa kwa mtu yoyote kukutwa au kutoa taarifa za takwimu zilizopatikana kwa kukiuka vifungu vya sheria vya takwimu kwani adhabu za kosa hilo ni kifungo kisichopungua miezi 12 au faini isiyopungua milioni tano au vyote kwa pamoja.

Dokta Chuwa ameyataja makosa mengine kuwa ni kutoa taarifa zisizo sahihi kwa msimamizi, mdadisi au karani wa sensa ikiwa ni pamoja na kumshawishi mtu yoyote asishiriki katika mchakato wa sensa kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha serikali kushindwa kupanga mipango ya maendeleo kwa wananchi wake.

 

Comments are closed.