WATANZANIA wametakiwa kujiepusha na vitendo vya rushwa kwani vitawafikisha pabaya na kurudisha maendeleo yao nyuma hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini-Takukuru, Dokta Edward Hosea katika mafunzo ya maafisa wa Taasisi hiyo juu ya utakatishaji fedha na kupata taarifa na mlolongo wa uhalifu kwa kutumia sheria za Tanzania.
Dokta Hosea amesema mafunzo hayo yatawasaidia maafisa hao kupata na kuelewa vithibitisho vya uhalifu vinavyogusa fedha na mali zilizopatikana kwa rushwa na kutaifisha mali chini ya sheria ya Tanzania ya utakatishaji wa fedha ya mwaka 2006.