WATANZANIA WANAKABILIWA NA CHANGAMOTO YAKUTOJUA SEHEMU SAHIHI ZA KUPATA HAKI ZAO

WATANZANIA WANAKABILIWA NA CHANGAMOTO YAKUTOJUA SEHEMU SAHIHI ZA KUPATA HAKI ZAO

Like
225
0
Friday, 31 July 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa bado kuna changamoto kubwa ya Watanzania wengi kutojua wapi wanaweza kupata haki zao jambo ambalo hata sehemu nyingine nje ya Tanzania wanalo.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angela Kairuki katika uzinduzi wa Mradi wa Elimu ya Uraia kwa njia ya Simu –PCC– ulioratibiwa na Asasi ya kiraia ya C-Sema- na Shirika la –UNIDEF- la Umoja wa Mataifa wenye lengo la kutoa elimu ya uraia kwa wananchi.

Akizungumza mara baada ya Uzinduzi huo Mheshimiwa Kairuki amesema Serikali imekuwa ikijitahidi kushirikiana na wadau mbalimbali kuangalia namna ambavyo Watanzania wanaweza kupata taarifa muhimu ili kuweza kufuatilia musauala yao na kuyapatia ufumbuzi wa mambo mbalimbali.

Comments are closed.