WATANZANIA WASHAURIWA KUFUATA TARATIBU ZOTE ZA UCHAGUZI

WATANZANIA WASHAURIWA KUFUATA TARATIBU ZOTE ZA UCHAGUZI

Like
187
0
Monday, 19 October 2015
Local News

ILI Kuhakikisha Amani inakuwepo hususani katika kipindi hiki  cha Uchaguzi mkuu October 25 watanzania wameshauriwa kufuata  sheria zote za uchaguzi kama zilivyoelezwa  na tume ya uchaguzi nchini na kuhakikisha kuwa hawafanyi matendo yoyote yatakayopelekea uvunjifu wa Amani.

 

Hayo yamesemwa  leo jijini Dar es salaam Katika vikao vya Kamati ya wabunge wa nchi za ukanda wa Maziwa makuu- ICGLR waliopo nchini kwa ajili ya kuangalia mchakato mzima wa uchaguzi unavyoendeshwa.

 

Rais wa kamati hiyo PETER OLE MOSITE ameeleza kuwa watanzania hawatakiwi kuwa   na hofu kuhusu haki katika uchaguzi na kwamba suala zima la tofauti za itikadi linatokea pia katika  nchi mbalimbali duniani na ni ishara  kubwa ya kwamba Demokrasia inakua nchini.

Comments are closed.