WATANZANIA WATAKIWA KUELEKEZA NGUVU KUENDELEZA TAALUMA YA SAYANSI, TEKINOLOJIA NA MAWASILIANO

WATANZANIA WATAKIWA KUELEKEZA NGUVU KUENDELEZA TAALUMA YA SAYANSI, TEKINOLOJIA NA MAWASILIANO

Like
225
0
Friday, 14 November 2014
Local News

WATANZANIA wametakiwa kuelekeza nguvu katika kuendeleza taaluma ya sayansi, tekinolojia na mawasiliano ili kuinua uchumi wa nchi kupitia ukuaji wa tekinolojia unaoendelea kwa kasi duniani.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa mawasiliano sayansi na tekinolojia Profesa MAKAME MBARAWA alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kutathmini mafanikio ya miaka minne yatokanayo na mpango wa maendeleo ya tekinolojia kwa msaada wa serikali ya Italia.

Aidha Profesa Mbarawa amesema katika kipindi hicho cha miaka mine, Tanzania imeshatengeneza wataalamu wengi katika fani hiyo hivyo ameyataka makampuni nchini kuwatumia wataalam wa ndani badala ya kuchukua wataalam kutoka nje.

 

Comments are closed.