WATANZANIA WATAKIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUSOMA VITABU

WATANZANIA WATAKIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUSOMA VITABU

Like
300
0
Wednesday, 27 January 2016
Local News

WATANZANIA wametakiwa kujenga utamaduni wa kusoma vitabu ili kukuza uwezo wa ufahamu na kuongeza ujuzi katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Wito huo umetolewa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Joice Ndalichako kwa niaba ya Rais dokta John Pombe Magufuli katika ufunguzi wa Maonesho ya vitabu yanayofanyika katika meli ya Logos Hope inayozunguka katika maeneo mbali mbali duniani kuhamasisha usomaji wa vitabu.

Profesa Ndalichako amewataka Walimu na wakufunzi wa shule na vyuo nchini kutembelea katika meli hiyo ambayo imetia nanga Jijini Dar es salaam itakayokuwepo kwa muda wa wiki tatu ili kuongeza uwezo katika utoaji wa elimu.

Comments are closed.