WATANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUWAWEZESHA WANANCHI WENYE KIPATO CHA CHINI

WATANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUWAWEZESHA WANANCHI WENYE KIPATO CHA CHINI

Like
218
0
Friday, 09 January 2015
Local News

WATANZANIA wametakiwa kuwa na moyo wa kushirikiana ili wananchi wenye kipato cha chini waweze kupata mahitaji muhimu ya Binadamu ikiwa ni pamoja na Makazi salama.

Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na Meneja Mtendaji Mkuu wa Chama Cha ushirika cha ujenzi wa Nyumba chenye makao makuu yake Mwenge jijini Dar es salaam THOMAS MOSHA alipozungumza na Waandishi wa Habari katika hafla ya kuwaapisha viongozi wapya wa Bodi ya chama hicho.

Ameeleza kuwa kitendo cha kusaidia wananchi wa kipato cha chini kupata makazi salama ni kuiunga mkono falsafa ya Rais wa kwanza wa Tanzania hayati Mwalimu JULIUS NYERERE.

Comments are closed.