WATANZANIA WATAKIWA KUZITUMIA FURSA ZA ELIMU

WATANZANIA WATAKIWA KUZITUMIA FURSA ZA ELIMU

Like
220
0
Tuesday, 17 February 2015
Local News

WATANZANIA hususani Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini wameshauriwa kutumia fursa zinazojitokeza katika kupata Elimu ili kutimiza malengo yao waliyojiwekea.

Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Dokta BENHADJ MASOUD wakati akifungua rasmi mpango wa utoaji wa fursa katika Elimu ulioshirikisha nchi za Afrika Mashariki na nchi za Scandinavia.

Dokta MASOUD amesema kuwa ikiwa mpango huo utatekelezwa ipasavyo utawasaidia kwa kiasi kikubwa Wananchi kutimiza malengo yao kupitia fursa zitakazopatikana.

Comments are closed.