WATATU MBARONI KWA WIZI WA VIFAA VYA TRANSFOMA DAR

WATATU MBARONI KWA WIZI WA VIFAA VYA TRANSFOMA DAR

Like
376
0
Friday, 04 September 2015
Local News

SHIRIKA la umeme nchini TANESCO kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamewakamata watu watatu wanaohusika na kuiba vifaa muhimu katika TRANSFOMA  mbili za wilaya ya Ilala na kupelekea wakazi wa maeneo hayo kukosa huduma ya umeme.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Tanesco, Ilala ATHANASIUS MANGALI, Amesema kuwa kumekuwa na wizi wa vifaa muhimu katika transfoma ambavyo vinapelekea kifaa hicho  kushindwa kusambaza umeme ipasavyo.

Amesema Tanesco kwa msaada wa karibu kutoka  jeshi la polisi jana majira ya usiku wameweza kuwakamata wahalifu hao na mpaka sasa wanashikiliwa na  polisi.

Comments are closed.