WATENDAJI WA SEKTA YA BIMA YA AFYA WATAKIWA KUONGEZA KASI YA KUHUDUMIA WAHANGA WA AJALI

WATENDAJI WA SEKTA YA BIMA YA AFYA WATAKIWA KUONGEZA KASI YA KUHUDUMIA WAHANGA WA AJALI

Like
215
0
Monday, 22 December 2014
Local News

WAZIRI wa Fedha Mheshimiwa SAADA MKUYA amewataka Watendaji wa Sekta ya Bima Nchini kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu yao kwa Wahanga wa ajali za Barabrani ambao wanazidi kuongezeka hivyo kuhitaji huduma ya haraka ya Kibima kutoka kwao.

Akizungumza na Waandishi wa habari   jijini Dar es salaam Mheshimiwa MKUYA amesema kumekuwa na ongezeko la ajali za barabarani ambazo zinazotokea kila sehemu jambo linalopelekea kupoteza Taifa la kesho ikiwa ni pamoja na watu kupata Ulemavu wa maisha kutokana na ajali hizo.

Amebainisha kuwa kwa mwaka 2013 jumla ya gharama zilizopatikana kwa ajali za barabrani zilikuwa Bilioni Tatu jambo linarudisha nyuma maendeleo ya nchi na Taifa kwa ujumla

Comments are closed.