WATOTO WAKUTANA KUJADILI MAPENDEKEZO KATIKA ILANI YA UCHAGUZI

WATOTO WAKUTANA KUJADILI MAPENDEKEZO KATIKA ILANI YA UCHAGUZI

Like
440
0
Monday, 14 September 2015
Local News

WATOTO  kutoka mabaraza mbalimbali nchini wamekutana Jijini Dar es salaam kwa lengo la kujadili na kutoa maamuzi juu ya masuala muhimu waliyoyapendekeza awali kuingizwa katika Ilani za uchaguzi.

 

Majadiliano hayo yametoa nafasi kubwa zaidi kwa watoto hao kuzichambua Ilani za vyama mbalimbali ambazo zinatumika katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu.

 

Akizungumza katika mkutano huo mkuu wa kitengo cha habari kutoka shirika la kusaidia watoto la Save The Children– ELLEN OTARU OKOIDION amesema kuwa majadiliano hayo pia yatasaidia watoto kuangalia ushiriki wa vyama vya siasa katika masuala muhimu ya watoto kupitia Ilani zao.

IMG_1970

Watoto wa Baraza hilo wakiwa makini kumsikiliza mwakilishi huyu

 

 

 

IMG_1980

 

pichani ni Mwakalishi wa Bodi kuu ya  ushauri watoto kutoka Zanzibar, Suhaila Msham Mwarimwana akizungumza na watoto wenzake kwenye baraza hilo

Comments are closed.