WATU 12 WAFARIKI KUTOKANA NA FOLENI YA MAGARI

WATU 12 WAFARIKI KUTOKANA NA FOLENI YA MAGARI

Like
358
0
Friday, 08 July 2016
Global News

Watu 12 wamefariki nchini Indonesia kutokana na foleni ya magari iliyosababisha mamilioni ya watu kukwama barabarani siku kadha.

Wengi walifariki kutokana na kukosa maji mwilini na uchovu.

Watu wengi waliokuwa wakisafiri kwa sherehe za kuadhimisha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan walikusanyika katika makutano ya barabara kisiwa cha Java.

Na hapo ndipo msongamano mkubwa wa magari ulipotokea.

Maafisa wa uchukuzi nchini Indonesia wanasema vifo hivyo vimetokea katika kipindi cha siku tatu.

Vyombo vya habari nchini Indonesia vinasema wengi wa waliofariki ni wazee ambao walikwama ndani ya magari chini ya joto kali.

Mtoto mmoja mchanga alifariki kutokana na kinachodhaniwa kuwa ni kupumua hewa chafu iliyojaa moshi wa magari.

Comments are closed.