WATU 2 WAUAWA MANDERA

WATU 2 WAUAWA MANDERA

Like
247
0
Monday, 28 December 2015
Global News

WATU wawili wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa baada ya wanajeshi kufyatulia risasi gari moja mjini Mandera katika hali ya kutatanisha.

Wanajeshi wamekuwa wakifanya operesheni kali mjini humo baada ya kuripotiwa kwa visa kadha vya mashambulio ya kigaidi siku za hivi karibuni.

Maafisa wanne wa polisi wameuawa kwenye mashambulio kadha katika mji huo ulioko kaskazini mashariki mwa Kenya katika kipindi cha wiki moja.

Comments are closed.