SERIKALI ya Venezuela imebuni mikakati ambayo itapelekea wafanyakazi wapatao milioni mbili wa serikali, kufanya kazi kwa siku mbili pekee kwa wiki katika kipindi cha majuma mawili.
Hatua hii inalenga kusaidia kukabiliana na uhaba wa umeme ambao unayumbayumba nchini humo.
Wafanyakazi hao wa umma na wale wanaofanya kazi katika sekta zinazomilikiwa na serikali watafika kazini siku za Jumatatu na Jumanne pekee hadi matatizo hayo ya nguvu za umeme yatakapodhibitiwa.