WATU LAKI NNE HUPOTEZA MAISHA KILA MWAKA KUTOKANA NA MABADILIKO YA HALI YA HEWA

WATU LAKI NNE HUPOTEZA MAISHA KILA MWAKA KUTOKANA NA MABADILIKO YA HALI YA HEWA

Like
281
0
Wednesday, 04 May 2016
Local News

INAKADIRIWA kuwa Watu laki nne hupoteza maisha kila mwaka Nchini kutokana na athari zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo mafuriko, ukame na migogoro ya rasilimali kwa Wakulima na Wafugaji.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Dokta Azma Simba katika Semina maalum ya Wanahabari iliyoandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Mamlaka ya hali ya hewa lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo Wanahabari kutoa elimu juu ya athari za mabadiliko ya tabia nnchi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Kinga ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dokta Simba amesema kuwa  mabadaliko ya hali ya hewa yameendelea kuleta athari kubwa katika Nyanja za kijamii, mazingira na afya ikiwemo ukosefu wa upatikanaji wa maji safi na salama.

Comments are closed.