WATU MILIONI TISA HUPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA UGONJWA WA SARATANI KILA MWAKA

WATU MILIONI TISA HUPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA UGONJWA WA SARATANI KILA MWAKA

Like
324
0
Wednesday, 04 February 2015
Local News

WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii Dokta SEIF RASHID amesema takribani watu Milioni Tisa wanakufa kila mwaka kutokana na kuugua ugonjwa wa Saratani.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri huyo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dodoma kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani ambayo huadhimishwa February 04 kila mwaka Duniani kote.

Ametaja kauli Mbiu ya mwaka huu kuwa ni UDHIBITI WA SARATANI UPO NDANI YA UWEZO WETU.

Amebainisha kuwa pamoja na idadi ya watu wanaokufa na ugonjwa huo kuwa kubwa lakini idadi hiyo na vifo itaendelea kuongezeka na kufikia Milioni 13 kwa mwaka ifikapo mwaka 2030.

 

 

Comments are closed.