WATU WAWILI WAPOTEZA MAISHA KWENYE SHAMBULIZI LILILOFANYIKA KATIKA CHUO CHA GARISA

WATU WAWILI WAPOTEZA MAISHA KWENYE SHAMBULIZI LILILOFANYIKA KATIKA CHUO CHA GARISA

Like
347
0
Thursday, 02 April 2015
Global News

WAPIGANAJI waliofunika nyuso zao wameshambulia eneo la Chuo Kikuu cha Garissa Kaskazini mwa Kenya karibu na mpaka wa Taifa hilo na Somalia.

Milio ya risasi pamoja na milipuko imesikika katika Chuo Kikuu cha Garissa mjini humo.

Maafisa wa Usalama wa Kenya wamethibitisha kuwa watu wawili wamefariki huku wanne wakijeruhiwa,huku wakaazi wa eneo hilo wametakiwa kukaa mbali na eneo la chuo hicho.

Haijulikani ni nani aliyekusika na shambulizi hilo ,lakini kundi la wapiganaji wa Somalia Al shabaab limetekeleza misururu ya mashambulizi mjini Garissa pamoja na maeneo mengine ya Kenya tangu mwaka 2011 wakati wanajeshi wa kenya walipopelekwa Somalia.

Comments are closed.