WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI KUJENGEWA KITUO KIKUBWA

WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI KUJENGEWA KITUO KIKUBWA

Like
278
0
Wednesday, 04 March 2015
Local News

TANZANIA kwa kushirikiana na Uturuki inatarajia kujenga kituo kikubwa cha watu wenye ulemavu wa Ngozi- albino,  ambacho kitakuwa na huduma mbalimbali muhimu ikiwamo shule na afya.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema kituo hicho kitawasaidia albino kupata huduma muhimu wakiwa kwenye mikono salama.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa kikao cha ndani cha mabalozi na wawakilishi wa nchi mbalimbali.

Waziri Membe amesema kituo hicho kitakuwa na watalaam wa kutoa mafunzo mbalimbali pamoja na ulinzi ikiwa ni mkakati wa serikali kuhakikisha tatizo la mauaji ya albino linakwisha nchini.

 

Comments are closed.